Taarifa za usafiri na malazi

Kama umepanda basi unatokea Dar es Salaam au mkoa mwingine wowote, tunashauri ushukie kituo cha Usa River madukani. Unaweza kupata usafiri wa teksi kuelekea chuoni MS TCDC au kwenye nyumba za kulala wageni kwa shilingi elfu 3,000/= mpaka
4,000/=. Kama umepanda ndege na unataraji kushukia uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), Arusha airport tunashauri uchukue teksi na umwambie dereva kuwa unashukia Denish (yaani Chuoni MS TCDC). Bei za teksi kutokea uwanja wa
ndege wa KIA ni shilingi 50,000/= na Arusha Airport ni shillingi 80,000/=. Pia unaweza kutumia usafiri wa mabasi ya kampuni ya shirika la ndege unalotaraji kusafiri nalo. Unaweza kupata bei zao kwa kuuliza shirika husika.

Kwa wasafiri wanaotokea Dar es Salaam tunawashauri kupanda mabasi yafuatayo:-
1. Kidia One
2. Dar Lux
3. Machame Trans
4. Kilimanjaro bus
5. Dar express
6. Tahmeed

Washiriki wote wa tamasha wanatarajiwa kufanya maandalizi ya malazi popote
watakapopenda Arusha mjini au Usa-River au Chuoni MS TCDC. Kwa msaada wa
kupata malazi unaweza kuwasiliana na hoteli au nyumba za wageni zilizoorodheshwa
hapa chini:-